Thursday, August 16, 2012

CAZORLA, FABREGAS WATUPIA HISPANIA IKISHINDA 2-1

Kocha wa Hispania kama vile alijua hawa jamaa watafunga akawachagua kuzungumza na vyombo kabla ya mechi yao dhidi ya Puerto Rico....   Wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Santi Cazorla (kulia) na Cesc Fabregas wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Carolina, Agosti 13, 2012. Timu hiyo itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Puerto Rico Islanders kesho. Picha: REUTERS

KIUNGO mpya wa Arsenal, Santi Cazorla aliifungia timu yake ya taifa ya Hispania katika ushindi wao wa wa 2-1 dhidi ya Puerto Rico usiku wa jana.

Cazorla na nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas walifunga magoli hayo wakati Hispania iliposhinda kirahisi dhidi ya Puerto Rico. Marc Cintron alipunguza goli moja kwa upande wa wenyeji katika dakika ya 65.

No comments:

Post a Comment