Friday, August 3, 2012

ANDY MURRAY KUMVAA FEDERER FAINALI YA KUWANIA MEDALI YA DHAHABU OLIMPIKI

Andy Murray akishangilia kutinga fainali ya tenisi ya Michezo ya Olimpiki baada ya baada ya kumshinda Novak Djokovic leo.
Mara ya mwisho walipokutana Murray alimwaga kilio... Roger Federer  akishingalia baada ya kumfunga Andy Murray katika fainali ya taji la Wimbledon mjini London Julai 8, 2012. Andy Murray (wa pili kulia) akiwa hoi.

Andy Murray akilia baada ya kufungwa na Federer katika fainali ya Wimbledon Julai 8, 2012.

MUINGEREZA Andy Murray atamkabili Roger Federer katika fainali ya Olimpiki ya tenisi kwa wanaume mmoja-mmoja Jumapili baada ya kumshinda Novak Djokovic kwa seti mbili mfululizo.

Murray alimchapa Mserbia huyo anayeshikilia Na.2 kwa ubora duniani 7-5 7-5 kwa kutumia saa mbili kamili katika Uwanja wa Wimbledon wa Centre Court na sasa amejihakikishia kutwaa angalau medali ya fedha.

Kikwazo baina ya Muingereza huyo na tuzo kubwa zaidi katika maisha ya yake ya tenisi, ni Federer, ambaye alimbwaga katika fainali ya Wimbledon Open.

Muingereza huyo alizungumzia kuhusu fursa ya kipekee ya kutwaa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki inayofanyika kwenye ardhi ya nyumbani na fursa hiyo sasa imewadia.

No comments:

Post a Comment