Wednesday, June 20, 2012


LEBRON JAMES AUMIA MIAMI IKINUSA UBINGWA NBA

Ajali....! James akipiga mwereka nyuma ya mlinzi wa Oklahoma City Thunder, Derek Fisher (37)
Yalaa...! James akisaidiwa kutoka nje ya uwanja baada ya kuumia.

 


MIAMI, Marekani
LICHA ya LeBron James kushuhudia dakika ya mwisho ya mechi akiwa benchi baada ya kuumia mguu na kutolewa nje akiwa amebebwa, nyota huyo aliisaidia Miami Heat kushinda kwa pointi 104-98 jana na hivyo kuongoza kwa 3-1 dhidi ya Oklahoma City katika mfululizo wa mechi zao saba za fainali ya Ligi Kuu ya Kikapu Marekani (NBA).
Ushindi huo umeifanya Miami ikaribie kutwaa taji la NBA kwani sasa watatakiwa kushinda mechi moja tu kati ya tatu zilizobaki.  
"Ni ushindi wa kusisimua sana," alisema LeBron, aliyefunga pointi 26, kucheza ribaundi tisa na kusaidia pointi 12.
LeBron alianguka na kuumia mguu wakati zikiwa zimesalia dakika tano kabla mechi kumalizika, huku Miami ikiongoza kwa pointi 92-90.

No comments:

Post a Comment