Friday, November 23, 2012

MLOPELO AFARIKI DUNIA, AZIKWA LEOMSANII aliyepata umaarufu mkubwa enzi za Kaole ya ITV, Mlopelo amefariki dunia mchana wa Alhamisi ya jana kwenye hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia aliyejitambulisha kwa jina moja la Azizi aliyeongea na tovuti ya Saluti5.com jana usiku, ni kwamba katika maisha yake yote, Mlopelo alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya mwili yaliyokuwa yakitulia na kuibuka tena hadi umauti ulipomfika.

Aziz amesema mazishi yalipangwa kufanyika Temeke leo Ijumaa saa 4 na kwamba msiba uko Temeke Wailes mtaa wa Boko.

Mungu amlaze mahala pema peponi.

No comments:

Post a Comment