Wednesday, October 10, 2012

RONALDO NA MESSI WANAWEZA KUCHEZA PAMOJA - GUTI


Guti
Lionel Messi wa Barcelona akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Real Madrid Jumapili Oktoba 7, 2012

Cristiano Ronaldo (kulia) akipongezwa na wachezaji wenzake wa Real Madrid baada ya kufunga dhidi ya Barcelona Jumapili Oktoba 7, 2012 katika mechi iliyoisha kwa sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Nou Camp.

MADRID, Hispania
JOSE Maria Gutierrez aka Guti, ametundika viatu vyake vya kuchezea soka, lakini jambo hilo halimaanishi kwamba ameupotezea jumla mchezo wa soka. Pamoja na kuwa mchambuzi wa soka katika kituo cha radio cha Cadena Cope, ameanza mafunzo ya kuja kuwa mkurugenzi wa michezo na pia anataka kuwa kocha.

Hapakuwa na maswali kuhusu kipaji cha soka alichokuwa nacho mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, na sasa anataka kujigawa na kuthibitisha uwezo wake katika kazi nyingine. Katika mahojiano yake, Guti alibainisha nini amekuwa akifanya hivi sasa na mipango yake ya baadaye.

Swali: Kwanini mkurugenzi wa michezo?

Jibu: Milango imefungwa katika kipindi changu cha kucheza soka, lakini sitaki kukaa mbali na soka. Kozi (ya kuja kuwa mkurugenzi wa michezo) inakupa mtazamo mzuri wa klabu nyuma ya pazia.

Swali: Kama maamuzi ya kwanza umeambiwa uchague baina ya Messi au Cristiano, utamsajili nani?

Jibu: Yeyote anaweza kuja. Wao wote ni wachezaji wa juu sana, wao ndiyo wachezaji bora duniani. Kama nitawapata wote, nitafurahi.

Swali: Lakini unadhani wanaweza kucheza pamoja?

Jibu: Ndiyo, kwa sababu hawachezi katika nafasi moja.

Swali: Unafikiri kocha bora anapaswa kuwaje?

Jibu: Yule ambaye anapenda mpira uchezwe unavyopaswa kuchezwa. Del Bosque, Michel, Laudrup na Schuster wanafiti katika falsafa hii.

Swali: Kama mkurugenzi wa michezo na, kutokana na uzoefu wako kama mcheza soka, nani utamchagua awe rais wako?

Jibu: Nitamchagua Florentino Perez. Anachokifanya kwenye klabu ya Real Madrid ni cha kipekee.

Swali: Kwa hiyo, mkurugenzi wa michezo, kocha au mchambuzi wa soka - nini utakachokifanya?

Jibu: Ninaenda vizuri katika kazi yangu ya uchambuzi wa soka kwenye radio na najifunza mengi. Hapa natumai nitaendelea kwa muda.

No comments:

Post a Comment