Mancini akiwa hoi baada ya kichapo. |
Yaya Toure wa Manchester City (kushoto) akilalamika kwa refa Kevin Friend |
Mata akipiga na kuifungia Chelsea dhidi ya Norwich leo Desemba 26, 2012 |
Mataaaaaaa....! |
MANCHESTER United iliendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa tofauti ya pointi saba leo baada ya kushinda 4-3 dhidi ya Newcastle wakati mahasimu wao Manchester City wanaowafuatia katika nafasi ya pili wakipata kipigo kisichotarajiwa cha bao 1-0 kutoka kwa Sunderland.
Ushindi wa Man U ulitokana na goli la dakika ya mwisho wa mechi lililowekwa wavuni na mshambuliaji Javier Hernandez "Chicharito" huku mabao mengine yakifungwa na Jonny Evans, Patrice Evra na Robin van Persie.
Man U walilazimika kutoka kuwa nyuma mara tatu 'kuibania' ushindi Newcastle.
Goli lililoimaliza Manchester City lilifungwa na straika wa zamani wa mabingwa hao wa England aliyeonekana hafai kwa kocha wao Roberto Mancini, Adam Johnson.
Hadi sasa, Man City wako nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nne tu dhidi ya Chelsea ambao walishinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Norwich City, mfungaji akiwa Juan Mata.
MATOKEO YA MECHI ZA LEO ENGLAND
Everton 2 Wigan 1
Fulham 1 Southampton 1
Man U 4 Newcastle 3
Norwich 0 Chelsea 1
Reading 0 Swansea City 0
Sunderland 1 Man City 0
No comments:
Post a Comment