Thursday, October 4, 2012

WAYNE ROONEY: JOE HART NDIYE KIPA BORA ZAIDI DUNIANI

Joe Hart
Joe Hart akiokoa shuti la karibu lililopigwa na Mario Gotze wa Borussia Dortmund wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters)
Duh... kweli Joe Hart kiboko...! - Straika Wayne Rooney wa Man U.
LONDON, England
STRAIKA nyota wa Manchester United, Wayne Rooney amesifu kiwango cha juu cha kipa wa mahasimu wao Manchester City, Joe Hart na kusema kwamba kipa anayeidakia pia timu ya taifa ya England ndiye bora zaidi duniani kwa sasa.


Rooney ametoa maoni hayo kufuatia kiwango cha juu kilichoonyeshwa na Hart jana usiku ambapo aliokoa mabao kadhaa ya wazi na kuisaidia klabu yake kuambulia sare ya 1-1 katika mechi ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, klabu ya Borussia Dortmund.


"Nadiriki kusema kwamba Joe Hart amekuwa katika kiwango cha kusisimua. Kwangu mimi, yeye ndiye kipa bora duniani kwa sasa," Rooney ameandika leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twiter.

No comments:

Post a Comment