Ronaldo akipiga shuti na kufunga goli la kwanza wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Amsterdam Arsena mjini Amsterdam, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters). |
Gervinho wa Arsenal akimtoka Giannis Maniatis wa Olympiacos wakati wa mechi yao ya Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, jana Oktoba 3, 2012. (Picha: Reuters) |
Weweeee....! Gervinho akishangilia goli alilofunga dhidi ya Olympiakos |
Lukas Podolski wa Arsenal akishangilia baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Olympiakos . |
Porto wakishangilia goli lao la ushindi dhidi ya PSG wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mjini Porto, jana Oktoba 3, 2012. |
Zlatan Ibrahimovic wa PSG akipiga kichwa kuelekea lango la Porto wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iliyochezwa mjini Porto, Ureno jana usiku Oktoba 3, 2012. |
Cristiano
Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos wameelezea furaha yao kutokana na ushindi walioupata
Real Madrid ugenini wa 4-1 dhidi ya Ajax na kusema kwamba wamepania kushinda
pia katika mechi ijayo ya ugenini dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Ronaldo alikuwa
shujaa wa kikosi cha Jose Mourinho baada ya kufunga ‘hat-trick’ huku bao jingine
likiwekwa wavuni na Karim Benzema, wakati Kaka na Sergio Ramos walipangwa
katika kikosi cha kwanza licha ya kuonekana kupoteza mvuto kwa kocha wao katika
siku za hivi karibuni.
"Nimefurahi
sana kwa sababu tumecheza vizuri na kushinda," Ronaldo ameiambia Canal+.
"Kwangu
mimi, kufunga mabao matatu ni muhimu. Tulicheza mechi vizuri sana na hilo ni
muhimu kwetu katika kujipa hali ya kujiamini kabla ya mechi yetu ijayo (dhidi
ya Barcelona). Ni muhimu sana kurejea nyumbani na mpira lakini ni muhimu zaidi
kwa timu nzima kwa sababu bila wenzangu nisingeweza kufunga magoli haya."
Barcelona inaweza
kuongeza tofauti ya pointi baina yao kufkia 11 kama itashinda dhidi ya Real
MadridJumapili, lakini Ronaldo anaamini kwamba timu yake ndiyo itakayoshinda.
"Ninajiamini
kwamba tutapata matokeo mazuri katika sehemu ngumu kushinda, ya Uwanja wa Camp
Nou. Wana timu nzuri sana na hakutakuwa na tofauti kubwa," alieleza Ronaldo,
ambaye magaoli yake matatu jana yalimfanya apate ‘hat-trick’ ya kwanza katika
ligi ya klabu bingwa Ulaya na pia kuongeza akaunti yake ya mabao katika
michuano hiyo kufikia 42.
Real sasa wanaongoza
katika kundi lao la D baada ya kufikisha pointi sita katika mechi mbili,
wakifuatiwa na Borussia Dortmund waliofikisha pointi nne baada ya kupata sare ya
1-1 katika mechi yao ya ugenini jana usiku pia dhidi ya Manchester City. Ajax
wanaburuta mkia baada ya kufungwa katika mechi zote mbili.
Nafasi ya Kaka
katika kikosi cha kwanza imekuwa ngumu msimu huu lakini kiungo huyo mchezeshaji
wa Brazili amejipanga kuhakikisha kwamba
anapata namba katika kikosi cha Real Madrid.
"Kidogo
ilinishangaza, lakini ni ushindi binafsi unaotokana na kujituma. Niko tayari
kwa kocha, vyovyote atakavyonihitaji.
"Barcelona
ni moja kati ya wapinzani wetu wa moja kwa moja, na hiyo inamaanisha kwamba
mechi dhidi yao ni muhimu sana."
Wakati
huohuo, baada ya ‘kuchenjiana’ hadharani na kocha wake Jose Mourinho, Sergio
Ramos amesema kwamba sasa wawili hao wamemaliza tofauti baina yao na nahodha
huyo msaidizi anaamini kwamba timu yake inaweza kuendelea na kasi yao ya
ushindi na kiwango kizuri uwanjani.
"Bifu
na Mourinho limeisha, na nimefurahia ushindi wetu katika Ligi ya Klabu Bingwa, jambo
ambalo ni la muhimu zaidi kwa timu," amesema beki huyo wa kimataifa wa
Hispania.
"Ulikuwa
ni ushindi muhimu dhidi ya timu ngumu, lakini sasa tunapaswa kugeukia La Liga. Mechi
ya Clasico inakuja na siku zote huwa ni maalum kwetu. Tunapaswa kuendelea na
kiwango hiki cha juu na kupata pointi nyingi zaidi katika ligi."
ARSENAL,
MILAN, PORTO SAAFI
Goli
lililofungwa na Mario Balotelli kuelekea mwishoni mwa mechi liliiokoa Manchester
City isifungwe nyumbani katika mechi yao dhidi ya Borussia Dortmund na kuambualia
sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Etihad jana.
Marco Reus
aliifungia Dortmund bao la utangulizi lililoelekea kuwazamisha wenyeji kabla mpira
uliopigwa na Sergio Aguerro haujagonga mkono wa Neven Subotic na refa kuwapa penati
iliyofungwa kiufundi na Balotteli katika dakika za lala salama.
Matokeo hayo
yaliifanya Man City iambulie pointi yake ya kwanza katika mechi mbili
walizocheza na hivyo kushika nafasi ya tatu kwenye kundi lao la D, wakiachwa
kwa pointi tano na vinara Real Madrid.
Arsenal
walijiimarisha kileleni mwa kundi lao la B baada ya kupata ushindi wa nyumbani wa
mabao 3-1 dhidi ya
Olympiakos.
Magoli
kutoka kwa Gervinho, Lukas Podolski na la ‘usiku’ kutoka kwa Aaron Ramsey ndiyo
yaliyowapa ushindi Arsenal na kubaki kileleni mwa kundi lao baada ya kufikisha
pointi sita, wakifuatiwa na Schalke wenye pointi nne.
Goli la Souleymane Camara katika dakika ya mwisho liliipa Montpellier
sare ya ugenini ya 2-2 dhidi ya Schalke na hivyo kuipa Arsenal uongozi wa
pointi mbili zaidi katika kundi lao la B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Montpellier walipata bao la utangulizi kabla wenyeji
hawajasawazisha kupitia Julian Draxler. Penati iliyofungwa na Klaas-Jan
Huntelaar ilionekana kuwapa ushindi Schalke kabla Montpellier hawajasawazisha
katika dakika ya mwisho kupitia kwa Camara na hivyo kuiacha Schalke ikibaki na
pointi nne.
Porto walikwea kileleni mwa Kundi A baada ya kupata ushindi
wa nyumbani wa 1-0 dhidi ya Paris St-Germain, ambapo goli hilo lilifungwa katika dakika ya 83 na mashambuliaji wao James Rodriguez.
Na goli la kujifunga kuelekea mwishoni mwa mechi kutoka kwa beki
Tomas Hubocan kuliigharimu Zenit St Petersburg na kujikuta wakilala nyumbani kwa
mabao 3-2 katika mechi yao dhyidi ya AC Milan.
No comments:
Post a Comment