Ramos akisikiliza maelekezo kutoka kwa Mourinho |
Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos amemuomba radhi kocha Jose Mourinho kwa kitendo chake cha kuvalia ndani jezi ya Mesut Ozil na kusaka goli kwa udi na uvumba ili ashangilie kwa kuionyesha kwa mashabiki kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mwishoni mwa wiki kwa nia ya kumuumbua kocha huyo.
Ramos hakufurahia kitendo cha Mourinho kumtoa Ozil na kumuingiza Kaka wakati wa mechi yao waliyoshinda 5-1 dhidi ya Deportivo La Coruna na hivyo alitaka kuonyesha hisia zake kwa kuonyesha jezi ya kiungo huyo wa Ujerumani, lakini akashindwa hata hivyo baada ya kutofunga goli.
Imeripotiwa na gazeti la Marca kuwa Ramos alimuomba radhi Mourinho mbele ya wachezaji wote na maafisa wa timu kwenye hoteli waliyofikia mjini Amsterdam, Uholanzi walikoshinda 4-1 dhidi ya Ajax na kusamehewa.
No comments:
Post a Comment