Chicharito: Dah! Hapa mambo yashakuwa magumu... lazima nisepe tu! |
Sikuja hapa kukalia benchi... lazima nisepe! -- Chicharito |
Nani |
Nani... safari inanukia! |
Straika wa timu ya taifa ya Mexico, Javier 'Chicharito' Hernández amekuwa akipata nafasi chache za kucheza msimu huu na kocha Alex Ferguson wa klabu yake ya Man U amemuweka katika orodha ya wachezaji atakaowapiga bei, pamoja na winga Nani, kwa mujibu wa shirika la habari la 'Bang Media International'.
Ferguson alimpanga Chicharito dhidi ya Cluj-Napoca katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya jana, ingawa alimtoa dakika chache kabla ya mechi kumalizika na kumuingiza Danny Welbeck.
Uwezekano wa Man U kumsajili straika Robert Lewandowski unaelezwa kuwa ni sababu ya kutakiwa kuuzwa kwa Chicharito.
Lewandowski alikuwa akifukuziwa na Manchester United na klabu nyingine kubwa za Ulaya katika dirisha la usajili uliopita wa majira ya kiangazi, na wasaka vipaji wa Man U watamfuatilia straika huyo leo katika mechi ya ugenini ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya klabu yake ya Borussia Dortmund na Manchester City.
Man U walitoa ofa ya kumnunua Lewandowski kwa euro milioni 20, lakini ombi lao lilikataliwa na mwishowe Man U wakaongeza nguvu katika kumsajili Robin Van Persie.
Pamoja na hayo, klabu hizo zimeendelea kuwasiliana wiki hii.
Lewandowski, ambaye ana mkataba wa kuichezea Borussia Dortmund hadi mwaka 2014 imeamua kutomuongezea mkataba wa kuendelea kucheza katika Bundesliga, Ligi Kuu ya Ujerumani na hivyo kumfungulia njia ya kuondoka katika usajili ujao wa majira ya kiangazi.
Ujio wa straika huyo utamuweka Chicharito katika nafasi ngumu zaidi ya kupangwa katika kikosi cha kwanza, ingawa hata sasa amekuwa akihaha kupata nafasi kwa Ferguson ambaye amekuwa akimuamini zaidi Welbeck.
Lewandowski pia atahatarisha nafasi ya Angelo Henríquez wa Chile kupata nafasi katika kikosi cha Man U kwani naye hucheza nafasi hiyo hiyo ya ushambuliaji wa kati.
No comments:
Post a Comment