Monday, September 3, 2012

ONA PICHA HIZI ZA "MAUGOMVI" YA KIM KARDHASHIAN

Tobaaa....! Mkao huu wa Kim Kardashian si ugomvi jamani?

Kim Kardashian... huu pia ni uchokozi. Sivyo?
NEW YORK, Marekani
Licha ya Kim Kardashian kuonekana kila mara akiwa beneti na "boifrendi" wake mwenye mihela kibao, msanii Kanye West, bado nyota huyo wa vipindi vya maisha halisi ya kwenye televisheni haishi vituko.

Hivi karibuni, Kim Kardashian aliposti picha za "kiuchokozi" kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, ambazo kwa kiasi kikubwa zilidhihirisha kuwa mrembo huyo mwenye umbile la kusisimua alipania hasa kuibua mihemko ya wanaume wakware.

Huku akiwa ametinga kinguo kinachoelezewa kirahisi kwa kimombo kama "sexy bikini", Kim Kardashian alipiga picha akiwa katika pozi kali la kwenye miamba na kuandika vijineno vyake vya "kiugomvi" kwa mtandao wake wa Twitter unaofuatiliwa na wafuasi zaidi ya milioni 16.

Katika picha ya kwanza, Kim Kardashian aliyevalia kivazi cha rangi ya dhahabu (gold monokini), alionekana amejibinua kidogo na kuacha midomo yake wazi huku pia akiwa kama anayeringia umbile lake la kuvutia, kisha akaandika: "Kukwea miamba...lol"

Katika picha ya pili, Kim Kardashian aliachia kwa makusudi vifungo vya kinguo chake kiduchu cha juu na kuanika matiti yake kimtindo. Hapa akaandika maelezo ya picha kwa maneno mawili: "Rock hard!".

Huu kama si ugomvi ni nini? Au anataka wakware wamuonee wivu Kanye West?

No comments:

Post a Comment