Hapa hupiti dogo...! Mikel Arteta wa Arsenal akichuana na Joe Allen wa Liverpool (kulia) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, leo Septemba 2, 2012. (Picha: REUTERS) |
LONDON, England
Arsenal wameanza kufanya kweli katika Ligi Kuu ya England kwa gharama za Liverpool baada ya nyota wao wapya Lukas Podolski na Santi Cazorla wote kufunga mabao yao ya kwanza tangu wajiunge kwenye klabu hiyo wakati wakishinda ugenini 'kiulaini' kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Anfield.
Sare mbili za 0-0 kufuatia mauzo ya straika Robin van Persie kwa klabu ya Manchester United ziliibua maswali kuhusiana na uwezo wa kufunga wa Arsenal lakini Podolski alijibu kwa kufunga bao safi kabla ya mapumziko na kuwapa uongozi wageni hao.
Mhispania Cazorla aliihakikishia Arsenal ushindi katika dakika ya 67 na kumuacha kocha mpya wa iverpool, Brendan Rodgers akibaki na pointi moja tu baada ya kikosi chake kucheza mechi tatu za ligi tangu atwae madaraka.
Arsenal, ambao bado hawajaruhusu goli msimu huu, wamepanda hadi katika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi tano huku Liverpool wakiendelea kuhaha katika nafasi ya nne kutoka mkiani.
No comments:
Post a Comment