![]() |
Ubungo terminal? Hapa ni wakati Essien alipotua na begi lake tu jijini Madrid jana kwa nia ya kukamilisha usajili wake Real Madrid. |
![]() |
Karibu kijana... nakuaminia, wee bado jembe la ukweli na hapa utatisha sana! Kocha Jose Mourinho wa Real Madrid akimkaribisha Essien |
![]() |
Si mnaiona jezi yangu? Hapa Essien akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari baada ya kukamilisha usajili wake Real Madrid jana. |
![]() |
Nimependedha eenh...! Essien akiwa na jezi ya klabu yake mpya ya Real Madrid. |
![]() |
Hapa Essien akiwa kwenye Uwanja wa Real Madrid wa Bernabeu baada ya kukamilisha usajili wake klabuni hapo jana. |
Maujuzi... Essien akionyesha utundu wake baada ya kutambulishwa Real Madrid jana. |
Nina usongo na hao Barcelona! |
![]() |
Hapa upendo tu..! Essien akitaniana na wenzake kwenye mazoezi ya Real Madrid jana. |
Kiungo wa kimataifa wa Ghana, Michael Esssien amesema kuwa amefurahi mno kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa muda mrefu kutoka Chelsea na kutua Real Madrid jana huku akiahidi kucheza kwa nguvu na uwezo wake wote ili kuisaidia timu hiyo kutimiza lengo la kutwaa kila taji msimu huu.
“Kuitwa na Mourinho ni zaidi ya furaha kwangu, yeye amekuwa kama baba yangu na niko tayari kucheza katika nafasi yoyote atakayoamua kunipanga; tuna uhusiano mzuri sana baina yetu”, amesema mchezaji huyo mpya wa Real Madrid, ambaye alitua Chelsea mwaka 2005 baada ya kusajiliwa na Mourinho ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa akiwaongoza mabingwa hao wa Ulaya .
Licha ya kutua jana tu na kukabidhiwa jezi namba 15, Essien alikwenda moja kwa moja mazoezini na kujifua na wenzake kabla ya kujumuishwa katika kikosi cha wachezaji 20 wa Real Madrid kitakachokuwa tayari kucheza leo saa 2:50 usiku kwa saa za Kibongo dhidi ya Granada katika mechi yao ya tatu ya msimu huu wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.
Wachezaji 20 waliojumuishwa kikosini na kocha Jose Mourinho leo ni:
Makipa: Casillas, Adán na Pacheco.
Mabeki: Sergio Ramos, Marcelo, Albiol, Pepe, Arbeloa na Varane.
Viungo: Özil, Xabi Alonso, Khedira, Essien, Modric, Callejón, Di María na Kaká.
Mastraika: Cristiano Ronaldo, Benzema na Higuaín.
No comments:
Post a Comment