Ommy Dimpoz "kwa pozi" (kushoto) akiimba wimbo wa "Nai Nai" aliomshirikisha Ali Kiba (kulia) katika moja ya maonyesho ya ziara ya washindi wa tuzo za Kili 2012. |
Ommy Dimpoz "kwa pozi" (kulia) akitumbuiza katika moja ya maonyesho ya ziara ya washindi wa tuzo za Kili 2012. |
MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayetamba na nyimbo zake mbili za 'Nai Nai' na 'Baadaye', na mshindi wa tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Ommy Dimpoz anataraji kuzindua video yake mpya ya 'Baadaye' katika ukumbi wa Club Maisha Septemba 9, 2012 jijini Dar es Salaam.
Meneja wa msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na shoo itakuwa ya kuvutia.
Mubenga amesema Dimpoz amerekodi video yake hiyo nchini Afrika Kusini.
Aidha, Mubenga amesema kuwa kazi ya utayarishaji wa video hiyo ulifanywa na Adam Juma wa Visual Lab ambaye ndiye walisafiri naye hadi Afrika Kusini na wamerekodi kwenye maeneo mazuri na ya kifahari yaliyopo nchini humo ambapo ameona utofauti mkubwa katika kufanya video nje na nyumbani.
“Kazi hii ni ya uhakika ambayo tunaizidua Jumapili hii na Video hiyo imefanyika Johannesburg mitaa ya Sendton na nikatika location kali na za uhakika,”alisema Mubenga.
Amesema wasanii kadhaa watasindikiza uzinduzi huo akiwepo Chegge Chigunda, Suma Mnazareth na Nas 3 siku hiyo katika uzinduzi wa video hiyo mpya na Dimpoz naye atakuwa katika muonekano tofauti si Dimpoz waliyemzoea.
Meneja huyo wa Dimpoz amesema akiwa nchini Afrika Kusini msanii huyo alimshirikisha mwanamitindo Tully Tshabalala, ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii wengi wakali wa muziki nchini.
“Wimbo ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongofleva wakae tayari kwa video hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya televisheni nchini na kumbi za burudani baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.
Mubenga amewakata wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumpa sapoti Dimpoz katika uzinduzi huo wa aina yake katika Club Maisha Oysterbay jijini la Dar es Salaam Jumapili.
No comments:
Post a Comment