Tuesday, September 4, 2012
MESSI ADHAMIRIA KUENDELEA KUJIKUBALISHA KWA MASHABIKI WA TAIFA ARGENTINA, TAYARI KESHAWAFUNGIA MABAO 9 KATIOKA MECHI 5
BUENOS AIRES, Argentina
TIMU ya taifa ya Argentina imeamsha mapenzi mapya kwa mashabiki wao kuelekea mechi yao ya Ijumaa ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Paraguay kufuatia kiwango cha nahodha wao Lionel Messi aliyefunga magoli TISA katika mechi TANO zilizopita.
Messi alifunga 'hat-trick' mara mbili katika ushindi dhidi ya Brazil na Uswisi na goli moja katika kila mechi dhidi ya Colombia, Ecuador na Ujerumani baada ya kuzomewa na mashabiki wao kufuatia sare yao ya 1-1 dhidi ya Bolivia Novemba mwaka jana.
"Tulijua kwamba tunapaswa kubadilisha mambo baada ya sare dhidi ya Bolivia," Messi aliuambia mkutano na wanahabari nchini Argentina leo.
"Tulijua kwamba tulihitaji kuwashawishi mashabiki kutokana na matokeo yetu na kiwango katika mechi zetu."
Argentina walianza mfululizo wa kushinda mechi tano ugenini dhidi ya Colombia siku nne baada ya fadhaa waliyoipata dhidi ya Bolivia, kwa kushinda wakitoka 2-1 nyuma kupitia magoli ya Messi na Sergio Aguero.
Ushindi wa 3-1 dhidi ya Uswisi mjini Berne ulifuatiwa ushindi wa kishindo wa 4-0 dhidi ya Ecuador mjini Buenos Aires katika mechi yao ya kufuzu iliyofuata mwezi Juni. Wakawafunga waandaaji wa fainali za Kombe la Dunia 2014 Brazil kwa magoli 4-3 katika mechi ya kirafiki mjini New Jersey wiki moja baadaye na wakawachapa Ujerumani mjini Frankfurt mwezi uliopita.
Mechi yao ijayo Ijumaa kwenye Uwanja wa Kempes mjini Cordoba unaochukua mashabiki 57,000 tayari umeshauza tiketi zote.
"Mashabiki wana matarajio na sisi pia. Tutarajie itakuwa poa kwa taifa na tupate pointi tatu," Messi alisema.
Messi anafahamu, hata hivyo, ugumu uliopo kuifunga Paraguay licha ya kucheza chini ya kocha mpya Gerardo Pelusso baada ya kumtimua Francisco Arce kutokana na namatoke mabaya.
"Daima wao ni wagumu, katika kiwango chochote walichonacho. Mechi za kufuzu ni ngumu sana," Messi alisema.
"Pengine wanakuja wakiwa hawako katika kiwango chao bora lakini tunajua ubora wa wachezaji walionao. Wao ni timu ngumu na watafanya maisha yawe magumu kwetu."
Argentina ni wa tatu katika Kundi la Amerika Kusini wakiwa na pointi 10 kutokana na mechi tano, pointi mbili nyuma ya vinara Chile, na pointi moja nyuma ya Uruguay, ambao wanaenda ugenini Colombia.
Paraguay, waliofika robo-fainali nchini Afrika Kusini 2010, wako pointi nafasi moja kutoka mkiani katika kundi hilo lenye timu tiwa wakiwa na pointi nne.
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment