Tuesday, September 4, 2012

RONALDO ADAIWA HAKUSHANGILIA ALIKUWA AKIOMBOLEZA MIAKA 7 YA KIFO CHA BABA YAKE, MAN CITY WAMUANDALIA 'MIHELA'

Cristiano Ronaldo

MANCHESTER City wako tayari kutuma maombi ya kutaka kumsajili mshambuliaji Cristiano Ronaldo ambaye hana furaha katika klabu yake ya Real Madrid kwa ada ya uhamisho itakayoweka rekodi duniani ya paundi milioni 95.

Gazeti la Daily Star limesema kuwa Man City wanaandaa mkataba "mnono balaa" wa miaka minne kwa ajili ya nyota huyo wa zamani wa Manchester United.


Kumnunua Ronaldo kutamlazimisha kocha Roberto Mancini kuuza wachezaji wengine kadhaa ili kufungua njia kwa ajili ya mshahara wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye analipwa akisi cha paundi 250,000 kwa wiki na klabu yake ya Madrid.


Hata hivyo jambo hilo, halitarajiwi kutimia hadi mwisho wa msimu, wakati Real watakapoona kwamba wanalazimika kumuuza nyota huyo ambayo kipengele cha kuvunjia mkataba wake ni kinasemekana kuwa ni euro bilioni 1.


Ronaldo ambaye hakushangilia wakati alipofunga magoli yake dhidi ya Granada Jumapili, aliwaandia waandishi wa habari baada ya mechi hiyo: "Sikushangilia kwa sababu sina furaha. Sina furaha kutokana na masuala ya kikazi na watu klabuni wanajua ni kwanini.


"Sina chuki dhidi ya Iniesta (kutwaa tuzo ya URFA). Sitazungumzia tena mambo haya na akili yangu nailekeza kwenye timu ya taifa Ureno kwa sasa. Kuna mambo muhimu zaidi ya hili."


Ronaldo amedaiwa kwamba ametofautiana na wachezaji wenzake katika chumba cha kuvalia akiwamo Marcelo.


Hata hivyo, imedaiwa kuwa Ronaldo hana mpango wa kuondoka klabuni hapo na kwamba hakushangilia magoli yale kwa kuwa aliyafunga katika siku ambayo alikuwa akikumbuka miaka saba ya kifo cha baba yake.


"Hakutaka kucheza mechi ile... aliomba kwa uongozi apewe siku kadhaa za kupumzika.. lakini menejimenti ilimlazimisha acheze. Ndio maana alikuwa amekasirika na hakushangilia alipofunga goli lake la 150 katika mechi 149 alizocheza tangu ajiunge na klabu hiyo. Baada ya mechi alilia kwa dakika 20 na kisha akaondoka uwanjani. Alijisikia vibaya sana kwa sababu baba yake alikuwa ni kila kitu kwake," kilidai chanzo.

No comments:

Post a Comment