Sunday, September 9, 2012

FABREGAS: SINA MPANGO WA KUHAMA BARCELONA

Cesc Fabregas

KIUNGO wa Barcelona, Cesc Fabregas amekanusha uvumi kwamba anataka kuondoka Nou Camp.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema ripoti zinakuzwa tofauti na ukweli ulivyo na kwamba anataka kuendelea kuzeekea Barca.

"Jambo hili lote linakuzwa," aliiambia Radio Catalunya.

"Nina furaha. Niko katika klabu ambayo kwa miaka tele nilitaka kuwapo. Kwa sasa nimetulia.

"Nafanya kazi yangu na kujituma kama wengine wote ili kumpa wakati mgumu kocha (kuniacha nje).

 
"Nataka kustaafu nikiwa Camp Nou."

No comments:

Post a Comment