Bingwa wa dunia wa ngumi za uzito wa juu wa taji la WBC, Vitali Klitschko (kulia) akimchapa mpinzani wake Mjerumani Manuel Charr wakati wa pambano lao mjini Moscow jana usiku Septemba 8, 2012. |
Bingwa wa dunia wa ngumi za uzito wa juu wa taji la WBC, Vitali Klitschko (kulia) akimchapa mpinzani wake Mjerumani Manuel Charr wakati wa pambano lao mjini Moscow jana usiku Septemba 8, 2012. |
Mjerumani Manuel Charr akijibu mapigo dhidi ya bingwa wa dunia wa ngumi za uzito wa juu wa taji la WBC, Vitali Klitschko (kulia) wakati wa pambano lao mjini Moscow jana usiku Septemba 8, 2012. |
Mjerumani Manuel Charr (wa pili kushoto) akipinga baada ya refa kusimamisha pambano lake dhidi ya Vitali Klitschko. Kabla ya kipigo cha jana, Charr alikuwa amepigana mara 20 na kushinda yote. |
Manuel Charr 'akilamba sakafu' katika raundi ya pili ya pambano lake aliloelemewa mno chini ya bingwa mtete wa taji la WBC la ndondi za uzito wa juu usiku wa kuamkia leo |
Baada ya hasira kupoa, Charr alirejea katika uungwana wa michezo na kumpa mkono mshindi Vitali Klitschko |
Nimekubali we mkali.... hapa hasira zimeisha. Manuel Charr (kushoto) akimpongeza Vitali Klitschko baada ya pambano lao |
BINGWA wa dunia wa ndondi za uzito wa juu wa WBC, Vitali Klitschko alimsambaratisha mapema mpinzani wake Mjerumani Manuel Charr, kwa TKO ya raundi ya nne mjini Moscow.
Klitschko (41) alipata ushindani mdogo mno kutoka kwa mpinzani wake huyo ambaye hapo kabla alikuwa hajawahi kupoteza pambano.
Bondia huyo wa Ukraine alimlambisha sakafu mzaliwa wa Beirut, Charr (27) kwa ngumi kali ya mkono wa kulia katika raundi ya pili.
Na Charr, ambaye ushindi wake unaokumbukwa zaidi ni dhidi ya Muingereza Danny Williams, alisimamishwa katika raundi ya nne kutokana na damu kumwagika kama maji kutoka chini ya jeraha alilopata chini ya jicho lake la kulia.
Alicharuka kwa hasira kufuatia maamuzi hayo - yaliyotokana na madaktari waliokagua jeraha hiyo - na akapinga matokeo kwa muda wote bila ya mafanikio.
Pambano la Klitschko lilikuwa ni la ushindi wa pointi dhidi ya Muingereza Dereck Chisora mwezi Februari, lakini mechi hiyo ilifunikwa na tukio la mkazi huyo wa London dhidi ya Muingereza mwenzake David Haye kuishia kutaka kuzipiga katika vurugu kubwa iliyozuka wakati wa mkutano na wana habari baada ya pambano.
Haye, ambaye alipigwa kwa pointi na mdogo wake Klitschko, Wladimir mwaka jana, alikuja kumpiga Chisora kwa KO Julai na tangu wakati huo amekuwa akisukuma mambo akitaka apigane na Vitali.
Kutokea kwa pambano hilo kutatarajia kama Klitschko hatastaafu na kuweka nguvu zake katika siasa.
Rekodi zao
Klitschko | Charr | |
---|---|---|
45 | Kushinda | 21 |
0 | Sare | 0 |
2 | Kupigwa | 1 |
41 | KO | 11 |
41 | Umri | 27 |
6ft 7in | Urefu | 6ft 3½in |
79in | Urefu wa mkono | 77in |
No comments:
Post a Comment