Safiiii...! Kutoka kushoto ni Pepe, Ronaldo na Nani. Hapa wanashangilia goli walilofunga wakati wa fainali za Euro 2012. |
Ronaldo alikataa kushangilia magoli mawili aliyoifungia klabu yake inayofundishwa na Jose Mourinho wakati wakishinda 3-0 dhidi ya Granada Jumapili iliyopita, akisema kkutokuwa kwake na furaha ndio sababu.
Lakini, Ronaldo (27), straika wa zamani wa Manchester United, 27, alishangilia bao lake la kusawazisha wakati Ureno ikishinda juzi 2-1 dhidi ya Luxembourg.
Baada ya mechi hiyo, Nani akasema: “Ronaldo yuko poa. Hamkumuona? Hana huzuni, yuko poa.”
No comments:
Post a Comment