Friday, August 17, 2012

MASHABIKI WA ARSENAL WAZIPIGA KIBERITI LEO JEZI ZAO ZOTE ALIZOKUWA AKIVAA ROBIN VAN PERSIE...!

Naichoma moto yote... kwanza straika mwenyewe ana miguu ya glasi... akiumia kidogo tu, ankaa nje nusu msimu! Shabiki huyu wa Arsenal akiendelea na kazi ya kuichoma moto jezi iliyokuwa ikitumiwa na straika Van Persie wakati alipokuwa akiichezea Arsenal.

Huyu Van Persie katusaliti sana.... tuchome moto jezi yake! Baadhi ya mashabiki wakiiteketeza kwa moto leo jezi iliyokuwa ikitumiwa na Van Persie wakati akiwa Arsenal

Baadhi ya jezi za Van Persie wakati akiwa Arsenal zikiwa tayari kuteketezwa zote kwa moto na mashabiki waliokasirishwa na uhamisho wake kwenda Man U. 

Mwana umefanya uamuzi wa akili sana.... ungebaki Arsenal usingebeba kombe hadi unazeeka...! Wayne Rooney (kulia) akifurahia jambo na Van Persie wakati mastraika hao wa Man U walipkuwa wakifanya mazoezi ya pamoja kwa mara ya kwanza kujiandaa na mechi yao ya Jumatatu dhidi ya Everton.
MANCHESTER, England
BAADHI ya mashabiki wenye hasira wa Arsenal wameonyesha kukerwa na kitendo cha nahodha wao wa zamani, Robin van Persie 'RVP'  kuhamia kwa mahasimu wao Man U na hivyo kuamua kuzipiga kiberiti jezi Na.10 za Arsenal ambazo alikuwa akizivaa straika huyo.

Straika huyo wa kimataifa wa Uholanzi alionekana kuwachefua zaidi baadhi ya mashabiki wa klabu yake ya zamani baada ya kusaini mkataba wa miaka minne kuichezea klabu ya Manchester United na kusema kwamba amefurahi kutua kwenye klabu yenye 'usongo' wa kutwaa mataji".


Kauli hiyo imechukuliwa kuwa ni 'dongo' dhidi ya klabu yake ya zamani inayofundishwa na Arsene Wenger kwani haijatwaa kombe lolote katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Kocha wa Man U, Sir Alex Ferguson amesema kuwa atampanga Van Persie katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England watakayocheza Jumatatu usiku dhidi ya Everton.

Awali, Man U walitangaza kkukamilisha usajili wa Van Persie kwa taarifa iliyosema: "Robin van Persie amekamilisha vipimo vya afya, ameridhia maslahi yake binafsi na kusaini mkataba wa kuichezea Manchester United kwa miaka minne hadi Juni, 2016."

No comments:

Post a Comment