Messi na Ronaldo wakionekana kuwa hoi katika mechi mojawapo ya el clasico kati ya Barcelona na Real Madrid. |
Messi (kulia) na Ronaldo wakisubiri kutangazwa kwa mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2008. Ronaldo alishinda, Messi akashika Na.2. |
Lionel Messi amepuuza madai kwamba yeye na nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo wana uhasama binafsi unaotokana na ushindani mkali baina yao.
Mshambuliaji huyo nyota wa Argentina mwenye miaka 25, alikuwa akiyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mechi ya kimataifa iliyochezwa jana usiku kati ya Argentina na Ujerumani jijini Frankfurt.
Alipoulizwa kuhusu Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (Ballon d'Or) na mahusianao yake na mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ndipo Messi alipopuuza uvumi kwamba kuna uhasama baina yao.
"Mimi na Cristiano (Ronaldo) hatuna ugomvi. Yote hayo ni madai yanayopikwa na vyombo vya habari. Sijawahi kushindana na Cristiano au kupigana dhidi yake," mshindi huyo wa Ballon d'Or 2011 alisema.
"Hakuna chuki yoyote baina yetu, sote tunaheshimiana tu, lakini ningependa kuona Iniesta au Xavi, ambao kwa miaka mingi wameshinda mataji mengi makubwa kama Kombe la Dunia na ubingwa wa Euro, kutwaa tuzo hii kama mimi nikichemsha.
"Ni wazi kwamba Ronaldo, ambaye ni mchezaji mkali, kama alivyo (Iker) Casillas, wamekuwa pia wakijadiliwa katika mbio hizi za kuwabia tuzo, lakini urafiki wangu na wachezaji wote ninaocheza nao timu moja unakuwa mbele."
Mvunja - rekodi Messi tayari ameshatajwa, akiwa na Iniesta na Ronaldo, kuwa wachezaji watatu watakaochuana kuwania Tuzo ya UEFA ya Mwanasoka Bora wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment