Tuesday, July 10, 2012

WAZIRI MKUU PINDA AFIWA NA BABA YAKE


*AKABIDHI KITI CHAKE BUNGENI KWA SAMWEL SITTA

Waziri Mkuu Pinda (kulia) akipeana mikono na Mhe. Sitta. Katikati yao ni Mhe. William Lukuvi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amefiwa na baba yake, imefahamika.
Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Jenista Mhagama alitoa taarifa hiyo bungeni mchana huu wakati akiahirisha kikao cha asubuhi cha mkutano uliokuwa ukijadili hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji.
Mhe. Jenista alisema kuwa Pinda hatakuwepo bungeni kwa vile amekwenda kushughulikia msiba wa baba yake. Akaongeza kuwa kwa sababu ya msiba huo, Waziri Mkuu amemteua Waziri wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni kuanzia leo (Julai 10) hadi Julai 15.

No comments:

Post a Comment