Tuesday, July 10, 2012
FID Q AACHA GUMZO WAJANJA TOUR MTWARA
Na Mwandishi Wetu
MSANII na mkali wa hip hop nchini, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q juzi alifunika katika shoo wa Wajanja Tour ya Vodacom iliyofanyika Mtwara na kusababisha mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo kukataa asishuke jukwaani.
Fid Q alipanda jukwaani majira ya saa kumi na moja na nusu baada ya Diamond kumaliza shoo yake, na akiwa stejini umati wa wana Mtwara ulilipuka kwa shangwe na kuwapa wakati mgumu mabaunsa waliokuwa wakisimamia shoo hiyo. Hata alipomaliza nyimbo zake mashabiki walipiga kelele kutaka aendelee kuimba na kumwita Ngosha! Ngosha! Ngosha! nakuanza kulisukuma basi alilopanda msanii huyo mpaka nje ya uwanja.
Wasanii wengine waliofunika katika shoo hiyo ni pamoja na Diamond, Shetta, Ney wa Mitego na Mabeste.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema kuwa Tour ya Wajanja wa Vodacom itafanyika siku ya Jumapili ya wiki hii Mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.
"Wajanja Tour sasa inaelekea kwa "waja leo waondoka leo" mkoani Tanga baada ya kufunika vilivyo mkoani Mtwara hivyo wakazi wa Tanga wajiandae kupata burudani kutoka kwa wasanii kibao watakaotumbuiza," alisema Nkurlu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment