Msanii maarufu nchini Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz akiongea na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola
uliofanyika katika kiwanda cha Coca-Cola Kwanza Mikocheni, Dar es Salaam leo (Julai 10, 2012). Wengine ni
Evans Mlelwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya umma wa Coca-Cola Kwanza
(katikati) na Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Feisal Baghazal. Diamond ni balozi
wa kampeni hiyo.
Wateja wa Coca-Cola kujishindia
fedha taslim hadi Sh. milioni 1
Dar es Salaam Jumanne, Julai 10, 2012 …. Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza leo
imezindua promosheni ambayo itawawezesha watumiaji wa vinywaji vyake
kujishindia zawadi za fedha taslim hadi Sh. milioni 1. Zawadi nyingine za fedha taslim
ni 500,000, 100,000, 50,000, 10,000, 5,000, 2,000, fulana na soda za bure.
Promosheni hii pia ni sehemu ya kampeni kabambe ya
Coca-Cola iliyozinduliwa mwezi Aprili ijulikanayo kama
sababu bilioni moja za kuthamini Afrika
inayowahamasisha wananchi hasa vijana kuwa wazalendo na kujivunia raslimali
mbali mbali ambazo nchi za bara la Afrika zimejaliwa kuwa nazo.
Promosheni iliyozinduliwa leo itadumu kwa muda wa
wiki sita na inafahamika kama Vuta
Mkwanja na Coca-Cola. Hii ni fursa nyingine ambayo inatoa nafasi
kwa kampuni ya Coca-Cola kuwa karibu zaidi na wateja wake walioko nchi nzima,
mijini na vijijini.
“Ni dhahiri kwamba promosheni tunayoizindua hivi leo
itasaidia kuboresha maisha ya Watanzania watakaobahatika kushinda zawadi za
fedha taslim hasa wale ambao watajishindia ile zawadi kubwa ya Sh. milioni 1”, anasema
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa Coca-Cola Kwanza Evans Mlelwa.
Alisema kwa miaka mingi, Coca-Cola imekuwa ikiendesha
promosheni za aina hii ambazo zinawawezesha wateja kujishindia zawadi za fedha
taslim na hivyo kusaidia kuwakwamua kiuchumi na promosheni hii ya “Vuta Mkwanja na Coca-Cola ina lengo hilo la kuwawezesha
wateja wa Coca-Cola kiuchumi”.
Ili kushiriki, wateja wanatakiwa kukunua vinywaji vya
jamii ya Coca-Cola vyenye ujazo wa 350ml na kuangalia chini ya kizibo ili kuona
aina ya zawaidi waliojishindia.
Wakati washindi wa fedha taslim kuanzia Tsh 2,000
hadi 10,000 watapewa zawadi zao pale pale kwa wauzaji, washindi wa kuanzia Tsh
50,000 hadi 1m watakabidhiwa zawadi zao kwenye kiwanda cha kilicho karibu.
Viwanda hivyo ni Kwanza, Bonite na Nyanza.
Mlelwa ametoa rai kwa wateja wa Coca-Cola na umma wa
Watanzania kwa ujumla kushiriki katika promosheni hii ili kujiweka katika
nafasi ya kuwa milionea mara moja kwa hisani ya Coca-Cola.
Amesisitiza nia thabiti ya kampuni ya Coca-Cola kuendelea
kuzalisha na kusambaza vinywaji vyenye ubora wa kimataifa. Vinywaji hivyo ni
pamoja na Coca-Cola, Fanta na Sprite.
No comments:
Post a Comment