Sugu |
Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph
Mbilinyi (CHADEMA) ameibua upya bungeni sakata la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Steven
Ulimboka kwa kutaka tume huru iundwe mara moja ili kuchunguza ukweli wa tukio
hilo.
Sugu alisema Serikali yenyewe
haiaminiki kuhusiana na sakata hilo na hivyo kuna umuhimu wa kuwa na tume huru.
Sugu aliibua sakata hilo jioni hii (dakika
chache) zilizopita wakati akichangia akichangia hoja ya Ofisi ya Rais
(Menejimenti ya Utumishi wa Umma); akisisitiza kuwa suala hilo ni muhimu
kufanyiwa kazi kwa minajili ya kutunza amani na utulivu katika nchi.
Hata hivyo, Sugu aliipata wakati mgumu
kutoka kiti cha mwenyekiti wa mkutano huo, Sylvester Mabuma, baada ya
kufananisha sakata la kutekwa na
kushambuliwa Ulimboka na vitendo vilivyokuwa vikifanywa na kikundi cha
'Janjaweed' cha Sudan ambacho kilikuwa kikitesa na kuwaua wananchi nchini humo.
Kabla ya kuzua soo hilo, Sugu alisema
kwamba anafahamu kuwa sakata la mgomo wa madaktari liko mahakamani, lakini yeye
anachozungumzia ni suala la kutekwa kwa Ulimboka ambalo lenyewe haliko
mahakamani na hivyo hakuna kikwazo katika kulijadili.
Alisisitiza kwamba iundwe tume kama ya
'Dk. Mwakyembe" (wakati wa sakata la Richmond) ili ukweli wa kila
kilichotokea kwa Ulimboka ufahamike na wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya
sheria.
No comments:
Post a Comment