Monday, July 2, 2012

MJAPANI AMUIGA BALOTELLI KUSHANGILIA

Ken Tokura, mshambuliaji wa timu ya Vissel Kobe ya Ligi Kuu ya Japan akishangilia kama Balotelli baada ya kufunga goli la shuti la umbali mrefu.

Mario Balotelli siku aliposhangilia kwa staili yake.
Picha iliyounganishwa kwa kompyuta ikimuonyesha Mjapani Ken Tokura (kulia) aliposhangilia bao lake akimuiga Balotelli (kushoto)

Shabiki wa soka wa Italia akipozi nyuma ya picha kubwa la Mario Balotelli kabla ya mechi yao ya fainali ya Euro 2012 dhidi ya Hispania usiku wa kuamkia leo.

BAADA ya mshambuliaji wa klabu ya Vissel Kobe, Ken Tokura kufunga goli kali lililokuja kuwa la ushindi dhidi ya mahasimu wao wa Ligi Kuu ya Japan (J-League), Kawasaki Frontale, kwa shuti la umbali mrefu la mguu wa kushoto, alivua shati lake na kuiga staili ya kushangilia kwa kupozi kama sanamu ya Mario Balotelli, huku akitunisha misuli.

Kama mshambuliaji namba tisa mwenzake Balotelli alivyolimwa kadi ya njano, Tokura mwenye umri wa miaka 26 pia alilimwa njano kwa kuvua shati wakati akishangilia.

Mshambuliaji wa Manchester City, Balotelli alitokea kuwa mmoja wa nyota walioacha kumbukumbu kwa kucheza katika kiwango cha juu zaidi katika fainali za Euro 2012 baada ya kuifungia Italia magoli yote mawili katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Ujerumani katika nusu fainali.

No comments:

Post a Comment