TIMU ya taifa ya Rwanda ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 inatarajia kuwasili Dar es Salaam leo mchana (Julai 13 mwaka huu) kwa ndege ya RwandAir kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ngorongoro Heroes.
Rwanda
yenye msafara wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20 itafikia hoteli ya
Sapphire. Mechi hizo zitachezwa Julai 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Chamazi na Julai 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa.
Ngorongoro
Heroes tayari iko kambini chini ya kocha Jakob Michelsen na msaidizi
wake Adolf Rishard kujiwinda kwa mechi hizo ambazo ni sehemu ya
maandalizi ya kuivaa Nigeria.
Mechi
dhidi ya Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya
kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Algeria
itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment