TUSKER
ya Kenya na Ports ya Djibouti zinawasili leo jioni kukamilisha idadi ya
timu kumi na moja zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Kagame
yanayoanza kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
za kesho ni APR ya Rwanda dhidi ya El Salam Wau ya Sudan Kusini
itakayoanza saa 8 kamili mchana na kufuatiwa na ya saa 10 kamili jioni
kati ya mabingwa watetezi Yanga na Atletico ya Burundi.
Timu
zote kutoka nje ya mazoezi zimeshapangiwa viwanja vya mazoezi ambapo
zitavitumia kwa mujibu wa ratiba ambayo imepangwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF). Makazi ya timu hizo na viwanja vya mazoezi ni
kama ifuatavyo;
Timu: Uwanja wa mazoezi: Accommodation:
APR (Rwanda) Mabibo Hostel - Marriott Hotel (Mabibo External)
AS Vita (Congo) University of Dar es Salaam - Chichi Hotel (Kinondoni)
Atletico (Burundi) Mabibo Hostel - Lunch Time Hotel (Mabibo Hostel)
Azam (Tanzania) Azam Complex - Azam Complex (Chamazi)
El Salam Wau (S. Sudan) Zanaki Sekondari - Rungwe Hotel (Kariakoo)
Mafunzo (Z’bar) Kinesi - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Ports (Djibouti) Kinesi - Rombo Green View Hotel (Sinza)
Simba (Tanzania) ……………………. – Vina Hotel (Mabibo Makutano)
Tusker (Kenya) Zanaki Sekondari - Rungwe Hotel (Kariakoo)
URA (Uganda) Loyola - Valentino Royal Hotel (Kariakoo)
Yanga (Tanzania) …………………. – ……………………….
No comments:
Post a Comment