Wednesday, July 11, 2012

RONALDINHO AJIHARIBIA DILI LA MABILIONI YA PESA

Ronaldinho akizungumza na waandishi wa habari wakati akitambulishwa katika klabu yaike mpya ya Atletico Mineiro huku akionekana kuwa na makopo ya soda ya Pepsi mwzi uliopita. Utambulisho huu ndio uliomtibulia dili la mabilioni.

Katika kipindi cha mwezi mmoja tu uliopita baada ya kuachana na Flamengo kutokana na madai ya kutolipwa mshahara wake, Ronaldinho sasa ndiye aliyepigwa chini akishutumiwa kuvunja masharti ya mkataba wake mnono dhidi ya kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola.

Mshindi huyo wa zamani wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, amejiharibia ‘dili’ hilo lililokuwa likimuingizia kila mwaka kiasi cha dola za Marekani 737,400 (Sh. bilioni 1.1.) ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tu tangu aingie mkataba huo uliopaswa kumalizika mwaka 2014.

Kilichomponza Ronaldinho, ni kitendo chake cha kuonekana kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa na makopo ya soda ya Pepsi, ambao ni wadhamini wa klabu yake mpya ya Atletico Mineiro.

Ronaldinho alifanya hivyo mwezi uliopita wakati wa utambulisho wake katika klabu yake ya sasa ya Atletico Mineiro

No comments:

Post a Comment