*ADAI FIDIA MIL.550, NDOA ILIPANGWA JUMAMOSI IJAYO
Dk. Slaa |
Bi. Josephine Mushumbuzi |
Dk. Slaa akiwa jukwaani na Josephine Mushumbuzi |
Hapa Dk. Slaa (kulia) akiwa na Rose Kamili |
Rose
ameomba pia kulipwa na wawili hao jumla ya Sh. Milioni 550, ikiwa ni fidia ya
kuvurugiwa ndoa yake (na Dk. Slaa) na kwamba katika malipo ya fidia hiyo, Dk.Slaa
amlipe Sh. milioni 50 na Josephine Sh. milioni 500.
Wakili
Joseph Thadayo ndiye aliyewasilisha maombi hayo kwa niaba ya Rose na kesi kupata
usajili namba 4/2012, huku Jaji Laurence Kaduli akipangwa kuisikiliza.
Rose
anadai kuwa Dk. Slaa ni mume wake halali tangu mwaka 1985. Anasema kuwa Juni
18, 1987, alizaa mtoto wa kwanza na Dk. Slaa waliyemwita Elimiliana Slaa na Septemba
23, 1988, wakapata mtoto wao wa pili waliyemwita Linus Slaa.
Alisema
kuwa hata hati zao za kusafiria zilionyesha kuwa wao ni mke na mume na kwamba,
katika kipindi cha kuishi pamoja, walichuma vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyumba
mbili za kuishi, moja iko Sinza jijini Dar es Salaam, namba 609 Block E na
nyingine katika Kijiji cha Gongali wilayani Karatu, iliyojengwa mwaka 2005.
Rose
anadai kuwa uhusiano wa ndoa yao ulianza kuyumba mwaka 2009 baada ya mumewe
huyo kuanza mahusiano na Mushumbusi ambapo tangu wakati huo amekuwa hatoi
matunzo kwa familia yao, ikiwa ni pamoja na kutowahudumia kwa mavazi na chakula.
Rose ametaka Mahakama Kuu imuamuru Dk.Slaa ambaye ni mlalamikiwa wa
kwanza kumlipa fidia ya Sh. Milioni 50 na mlalamikiwa wa pili amlipe milioni
500, na kwamba wawili hao (Dk. Slaa na Josephine) wasiruhusiwe kufunga ndoa ya
aina yoyote.
No comments:
Post a Comment