Hapa Rais Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo ya taifa itakayoshiriki Olimpiki, leo jijini London. |
Rais JK akizungumza leo jijini London na wachezaji na maafisa wa timu ya taifa itakayoshiriki Olimpiki. |
JK akiteta leo jijini London na Balozi Kallaghe wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa itakayoshiriki Olimpiki. |
LONDON,
England
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, leo amekutana na
wachezaji sita wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya michezo mbalimbali iliyopo
jijini London kushiriki michezo ya Olimpiki kuanzia Julai 26.
Katika
mazungumzo hayo, Rais JK aliyekuwa na mkewe, Mam Salma Kikwete, aliwapa moyo
wachezaji hao na kuwataka wajitahidi kupeperusha vyema bendera ya taifa na
ikibidi warejee nchini na medali. Rais JK yupo England kwa ziara ya kikazi.
No comments:
Post a Comment