Mwalimu
wa warembo wa shindano la kumsaka Miss Sinza 2012, Mwajabu Juma, akitoa
maelekezo kwa warembo hao wakati wa mazoezi yao ya mwisho kujiandaa na
shindano hilo litakalofanyika kesho katika
Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hoteli, Sinza. Shindano hilo
litasindikizwa na burudani kabambe na shoo ya kufa mtu kutoka kwa Bendi
ya African Stars, watakaokuwa wakitambulisha pia baadhi ya nyimbo zao
mpya kwa mara ya kwanza, pamoja na msanii wa Vichekesho kutoka kundi la
Ze Commedy linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya Chanel 5,
Masawe Mtata, ambaye pia atakuwa akitambulisha video ya wimbo wake mpya
uitwao Uongo Kweli.www.sufianimafoto.blogspot.com
Warembo
hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao
litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan
Hotel.www.sufianimafoto.blogspot.com
Warembo
hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao
litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social,
karibu na Vatcan Hotel.www.sufianimafoto.blogspot.com
Warembo
hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao
litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan
Hotel.www.sufianimafoto.blogspot.com
Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.www.sufianimafoto.blogspot.com
Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao. www.sufianimafoto.blogspot.com
**********************************
MASHINDANO ya kumsaka mrembo bora wa Kitongoji cha Sinza, Redds Miss Sinza 2012 yatafanyika kesho (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho pamoja na kuwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali ya taji na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia zawadi ya Sh. 500,000 katika mashindano hayo yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’ ambao watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya. Pia atakuwepo msanii wa vichekesho wa kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa akitambulisha video na wimbo wake mpya wa "Uongo Kweli".
Akizungumza na mtandao huu, mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi nyingine kuwa ni Sh. 400,000 kwa mshindi wa pili, Sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu. Mshindi wa nne na wa tano watapata Sh. 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata Sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Aidha Majuto, aliongeza kuwa mbali na miondoko ya ‘catwalk’ jukwaani kutoka kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo watachuana ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012, ambapo mshindi atapata Sh. 50,000 kutoka mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi yamekamilika na viingilio vitakuwa ni Sh. 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa kitongoji cha Sinza wapate fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema Majuto.
Majuto aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa ni pamoja na Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith Sangu, Eva Mushi, Vailet John na Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com, Brake Point, Fredito Entertainment, Screen Masters, Lady Pepeta na flexi.
No comments:
Post a Comment