Hoi! Lionel Messi wa Barca (kushoto) na Cristiano Ronaldo wakionekana kuchoka kama majogoo yaliyotoka kuzipiga katika mechi mojawapo ya 'el clasico' misimu miwili iliyopita. |
REAL
Madrid na Barcelona zitakutana katika mechi yao ya kwanza ya
"Clasico" katika La Liga, Ligi Kuu ya Hispania mwishoni mwa wiki ya
Oktoba 6-7 kwenye uwanja wa Barca wa Nou Camp, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa
na Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) mjini Madrid leo.
Mabingwa
Real baadaye watawakaribisha Barca, ambao walimaliza katika nafasi ya pili
kwenye msimamo wa La Liga msimu uliopita, katika mechi watakayovaana mwishoni
mwa wiki ya Machi 2-3, RFEF ilisema.
Mahasimu
hao wa jadi watakutana mara mbili mwezi ujao katika mechi ya kuwania taji la
Hispania la Super Cup, ambalo litawakutanisha mabingwa wa La Liga (Real) dhidi
ya mabingwa wa Kombe la Mfalme (Barca).
Mechi
yao ya kwanza itachezwa Agosti 23 kwenye Uwanja wa Nou Camp, huku marudiano
kwenye Uwanja wa Bernabeu yakiwa Agosti 30, kwa mujibu wa taarifa ya RFEF.
Real
wataanza kampeni zao za kuwania ubingwa wa La Liga kwa kucheza nyumbani dhidi
ya Valencia, walioshika nafasi ya tatu
katika ligi hiyo msimu uliopita, ambapo watacheza mwishoni mwa wiki ya Agosti
18-19, wakati Barca wataanza kwa kuwakaribisha Real Sociedad.
"Utakuwa
msimu mgumu, kama ulivyokuwa msimu uliopita, na tutajaribu kufikia matarajio ya
mashabiki wetu," Mkurugenzi wa Real, Emilio Butragueno alisema wakati wa
upangaji ratiba.
Real
ya
kocha Jose Mourinho iliweka rekodi kwa kufikisha pointi 100 wakati
ikitwaa
ubingwa kwa mara ya kwanza msimu uliopita baada ya kupita misimu minne,
na kuhitimisha utawala wa Barca waliokuwa wametwaa ubingwa wa La Liga
katika misimu
mitatu mfululizo.
No comments:
Post a Comment