Dk. Mkopi (kushoto) akisindikizwa kuingia mahakamani leo |
Rais
wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), leo amefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili yanayohusiana na mgomo wa
madaktari na kusomewa mashtaka mawili kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
Makosa
aliyoshtakiwa nayo bosi huyo wa MAT ni ya kupuuza amri halali ya kusitisha
mgomo na jingine ni la kuhamasisha mgomo huo.
Ilidaiwa
mbele ya Hakimu Faisal Kahamba kuwa,
kati ya Juni 26 na Juni 28 mwaka huu, Mkopi alipuuza amri halali ya
Mahakama Kuu (Divisheni ya Kazi), ya kuzuia mgomo wa madaktari na badala yake kuhamasisha kuendelea kwa mgomo
huo kinyume cha sheria.
Rais
huyo wa MAT alichiwa na Hakimu Kahamba baada ya kutimiza masharti ya dhamana,
ambayo ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili waliomdhamini kwa Sh. 500,000 kila
mmoja.
Kesi
hiyo ambayo imeahirishwa hadi Agosti 6, ilivuta hisia za watu wengi ambapo mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam
walifurika mahakamani hapo, wakiwemo madaktari walioonekana kumuunga mkono rais
wao.
No comments:
Post a Comment