|
Mwaaa! Mabusu kwa kwenda mbele kati ya Iniesta na mkewe Anna... safi hiyo! |
|
Iniesta mwenye kumiliki bonge la kiwanda cha mvinyo akipata vitu f'lani na mkewe Anna baada ya kugongeana glasi |
|
Straika Messi akosekane? Nani kasema. Labda uulize naye ataoana lini na mrembo wake huyu? Hapa 'jini' akiwa ukumbini na mpenzi wake kuwahi mnuso wa swahiba Iniesta . |
|
Straika Pedro pia alikuwepo ukumbini na laazizi wake... si mnuso wa kitoto ati! |
|
Straika Samwel Eto'o na mkewe pia walikwea pipa kutoka Moscow nchini Urusi hadi Hispania ili kufaidi mnuso wa shwahiba wake Iniesta. |
|
Haloo...haloooo! Iniesta na mkewe wakimeremeta baada ya kuoana |
|
Mshumu... mshumu, mshumu tena... MWAAAAAAAAA!!!!! |
|
Hapa picha sijui ilitaka kuungua... mbayaaa! Lakini wanaoonekana ni pamoja na Gerard Pique (kushoto) na nahodha wa Barcelona, Cares Puyol (kulia). Wote walitupia mijumba kuwahi mnuso wa harusi ya mshkaji wao Iniesta. |
|
Cesc Fabregas (kulia) hakukosa kwenye mnuso huo na kimwana wake... in short, wengi walifika na mademu zao isipokuwa wachache kama Gerard Pique ambaye mpenziwe Shakira ni mjamzito. |
|
Super Mario Balotelli na masela wake kibao wa Italia pia walihudhuria mnuso huu. Si unawaona mwenyewe wazee wa 'pura maraka msosi pliiiizzz...! |
HISPANIA
Sherehe za harusi iliyofanyika jana ya
kiungo Andres Iniesta wa Barcelona na mpenzi wake wa ‘longtaim kitambo’, Anna
Ortiz ilihudhuriwa na wageni takriban 700, wakiwemo mastaa mbalimbali, hasa wa
soka.
Wapendanao hao walioana Tamarit katika
jimbo Tarragona, ambapo miongoni mwa mastaa wa soka waliohudhuria sherehe hizo
ni nyota wenzake wa soka kama Lionel Messi, Xavi Hernandez, Iker Casillas,
Carles Puyol, Gerard Pique, Cesc Fabregas, Pedro, Samuel Eto’o na Mario
Balotelli.
Hata hivyo, Pique alitinga kwenye
sherehe hizo akiwa peke yake baada ya kumuacha ‘mahom’ kwao mpenziwe Shakira
ambaye hivi sasa ni mjamzito.
Baada ya harusi hiyo, Iniesta aliandika
katika ukursa wake rasmi wa kijamii wa Twitter, ambao unafuatiliwa na mashabiki
milioni 4 duniani, akisema:
“Un dia increible! Recién casados. Ni
siku ya aina yake! Nimeoa.”
Mwisho wa ujumbe huo kwenda kwa
mashabiki wake wanaomfuatilia kupitia Twitter, Iniesta akatupia picha zake za
ndoa na mkewe Anna Ortiz.
No comments:
Post a Comment