Monday, July 2, 2012
AFANDE, AY WAPAGAWISHA TAMASHA LA COCA COLA MWANZA
VIJANA kutoka kona mbalimbali za jiji la Mwanza wamejitokeza kwa wingi kushiriki tamasha la Coca-Cola lijulikanao kama "Sababu Bilioni Moja za Kuithamni Afrika" likiwa na lengo la kuwahamasisha vijana na wananchi kwa ujumla kujiamini na kuipenda nchi yao na Afrika kwa ujumla.
Tamasha hilo la aina yake liliandaliwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottlers yenye makao yake hapa mjini Mwanza ambapo kivutio kikubwa katika tamasha hilo kilikuwa ni wasanii wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya Bongo Flava, Ambwene Yesayah marufu kama AY na Selemani Msindi a.k.a Afande Sele ambao waliwafanya maelfu ya vijana kusukumana huku na kule ili kupata nafasi nzuri ya kuwaona wanamuziki hao machachari wakifanya mambao jukwaani.
Katika tamasha hilo pia baadhi ya wasanii chipukizi walipata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao walipojimwaga uwanjani kuimba na kucheza pamoja na wasanii hao.
Aidha vijana hao pamoja na kuipongeza kampuni ya Nyanza Bottlers kwa kuona umuhimu wa kuandaa tamasha hilo, wamezitaka kampuni nyingine kuona umuhimu wa kusaidia kuibua vipaji vya vijana.
Kwa upande wao wasanii hao chipukizi wa Bongo Flava pamoja na kuipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa tamasha hilo na mengine yanayoigusa jamii hasa vijana a wameendelea kusema kuwa kampeni hii ya "Sababu Bilioni Moja za Kuithamini Afrika" imekuja wakati mwafaka na itasaidia kuhamisisha uzalendo miongoni mwa vijana.
Akizungumza katika tamasha hilo Meneja Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Alfred Malandu amesema Nyanza Bottlers kupitia kinywaji chake cha Coca-Cola itaendelea kuhamasisha jamii kujivunia na kutumia vitu vinavyopatikana Afrika.
Tamasha hilo pamoja na burudani mbalimbali ikiwemo muziki kulikuwa na michezo mbalimbali kama vile shindano la kupiga danadana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment