Tuesday, July 10, 2012

MATUMLA APAA USIKU HUU KWENDA KUZIPIGA UJERUMANI

Matumla (kushoto) akimpa mazoezi muigizaji Wema Sepetu kwa ajili ya pambano la hisani dhidi ya muigizaji Jacqueline Wolper lililofanyika Jumamosi ambapo Matumla alikuwepo ulingoni pia kumuongoza Wema.

Na Mwandishi Wetu
BONDIA gwiji nchini Tanzania, Rashid Matumla 'Snake Man' anasafiri usiku huu kwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya kwenda kupambana na bondia wa huko, Benjamin Simon.


Kwa mujibu wa mratibu wa ziara hiyo, Ali Bakari 'Championi', Matumla anaenda kuwania mkanda wa IBF katika pambano la uzani wa Supermiddle la raundi 12.


"Matumla anaondoka usiku huu. Atapandia ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya na atapigana na Benjamin Simon Jumamosi Julai 14. Atarudi hapa Julai 17," alisema Championi.

Championi ambaye ni bondia wa zamani na pia ni refa wa mchezo huo, alisema Matumla aliwahi kupigana na Simon mwaka 2010 lakini alipoteza pambano hilo kwa pointi.


"Hili ni pambano kubwa sana kwa matumla," alisema Championi kuhusu bondia huyo veterani alishatangaza kustaafu kupigana kabla ya kurejea tena ulingoni.

No comments:

Post a Comment