Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai |
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amelazimika kuahirisha
kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea jioni hii hadi kesho saa 3:00 asubuhi baada
ya taa zote za ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kuzimika ghafla na
kusababisha giza kubwa kiasi cha kuibua hofu.
Tukio hilo limetokea wakati Bunge lilipokaa kama kamati ili
kupitisha vifungu vya makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baada ya taa hizo kuzimika, Mhe. Ndugai akalazimika kuahirisha
zoezi lililokuwa likiendelea la kupitisha vifungu na Bunge likarejea katika
hali yake ya kawaida kabla naibu spika huyo hajatoa hoja ya kuahirisha kikao hicho hadi
kesho asubuhi.
Kabla ya hapo, tayari wabunge walishaanza vituko kwa kupeana
vijembe gizani, baadhi wakiwaita wenzao kuwa ni “wanafiki” na wengine wakituhumiana
kwa utani juu ya madai kwamba wamefanya hujuma ili kutibua kikao hicho.
No comments:
Post a Comment