Rais wa CWT, Gratian Mukoba |
RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba,
ameibuka leo na kupinga taarifa iliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu,
Kassim Majaliwa, aliyesema kwamba walimu hawana mgogoro wowote na serikali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mukoba amesema kwamba
kauli hiyo ya serikali bungeni si ya kweli kwani hivi sasa wana mgogoro na serikali
kuhusiana na madai yao mbalimbali.
Amefafanua kuwa mgogoro wao na serikali ulisainiwa tangu Juni
8 mwaka huu na kwamba, majadiliano yao na serikali hayajafikia muafaka baada ya
wenzao (serikali) kuomba kuahirisha hadi Julai 20.
Akaongeza kuwa, kama wakishindwa kuafikiana katika kikao chao
kinachofuata, watasaka idhini ya kuchukua hatua zaidi.
Mukoba aliita taarifa hiyo ya serikali kuwa ni ghilba na
kwamba kamwe haiwezi kuwasaidia walimu waliokosa mshahara na pia hazitasaizidi
kuinua morari ya walimu waliokata tamaa. Akasisitiza kwamba cha muhimu ni
kutanguliza ukweli na sio ghilba.
Hata hivyo, aliwataka walimu kuendelea na kazi katika kipindi hiki wanachoendelea kuzungumza na serikali.
Hata hivyo, aliwataka walimu kuendelea na kazi katika kipindi hiki wanachoendelea kuzungumza na serikali.
.
No comments:
Post a Comment