Monday, July 9, 2012

MANCINI ASAINI MKATABA MIAKA MITANO MAN CITY

Roberto Mancini siku alipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England.

KOCHA Roberto Mancini amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.

Mancini (47) alijiunga na Man City Desemba 2009 akichukua nafasi ya Mark Hughes (ambaye hivi sasa ni kocha wa QPR), na akaiongoza kutwaa Kombe la FA mwaka 2011.

Mwaka mmoja baadaye, Mancini akaiongoza Man City kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya England tangu mwaka 1968.

"Manchester City ni bonge la klabu," Mancini aliiambia tovuti ya klabu hiyo. "Niko kikamilifu kuangalia changamoto zinazokuja mbele."

"Nina furaha kuweza kutoa juhudi zangu zote kwa Man City kwa miaka mingine mitano.Fursa iliyopo katika kujenga timu kutokea katika mafanikio tuliyonayo sasa ni kipekee.

Mancini alileta Kombe la Ligi Kuu ya England katika siku iliyojaa "drama" ya mwisho wa msimu wakati goli la dakika za majeruhi ya Sergio Aguero kuwapa ushindi wa 3-2 dhidi ya QPR na kutwaa ubingwa kwa tofauti ya magoli dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United.

Ubingwa wa Man City uliongezea mafanikio katika ajira yake iliyopita klabuni Inter Milan, ambako alitwaa ubingwa wa Serie A kwa miaka mitatu mfululizo.

Mkataba huo umezima uvumi uliomuhusisha Mancini na mipango ya kwenda kuchukua nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Urusi kufuatia kuondoa kwa Dick Advocaat baada ya fainali za Euro 2012.  

No comments:

Post a Comment