UGOMVI, NGUMI ZATAWALA BIG BROTHER
Washiriki waletewa daktari wa saikolojia
Rapa wa Kenya, Prezzo (kushoto) akijiachia rafikiye wa kike wa ndani ya jumba la Upville la Big Brother StarGame, muimbaji wa Nigeria, Goldie. |
BAADA ya wiki nne za mivutano na ugomvi, Big Brother ameandaa daktari wa saikolojia kwa ajili ya kuwasaidia washiriki wa shindano hilo kwenye nyumba ya Upville.
Washiriki walizungumza kwa kirefu na daktari huyo katika muda maalum wa faragha kwenye sebule ya Upville.
Katika siku 14 zilizopita, washiriki WANNE wametimuliwa kutoka katika shindano hilo baada ya majibizano yao makali kugeuka kuwa ugomvi wa ngumi.
Kumekuwa pia na mkanganyiko mkubwa kwenye nyumba ya Upville tangu Maneta na Roki walipotimuliwa kama shoo ya kutolewa kwa washiriki Jumapili itafanyika kama kawaida ama haitakuwepo kufuatia kutolewa kwa wawili hao.
Big Brother kisha akawapa majibu ya maswali yao kwamba licha ya Maneta na Rookie kufukuzwa shindanoni, shoo ya kutoa washiriki itaendelea Jumapili kama ilivyopangwa.
Kimwana Mnigeria Goldie (kushoto) akiwa na Keitta, ambaye amemwingiza kwenye "chekeche" la kupigiwa kura za kutolewa mjengoni baada ya kumuokoa boifrendi wake wa ndani ya jumba, Prezzo wa Kenya. |
Jumatatu, Prezzo, Maneta na Barbz waliingia katika chekeche la wanaotakiwa kupigiwa kura ya kutoka mjengoni, lakini, Goldie alitumia nguvu yake ya kuwa Mkuu wa Nyumba kumuokoa boifrendi wake Prezzo na kumweka Keitta kwenye chekeche hilo.
Goldie hata hivyo alilia wakati akizungumza katika chumba maalumu cha kupiga stori na Biggie cha "Diary Room" na akabainisha kwamba anaumia kujiona kwamba amemsaliti shogaye, Barbz!
Talia ambaye aligombana na dada yake Tamara katika chumba cha kuchati na Biggie cha Diary Room. |
Katika nyumba nyingine ya Downville, ugomvi ulizuka kwenye chumba cha kuchati na Biggie baina ya mtu-na-dada-yake, Talia na Tamara.
Tamara alilalamika kuwa hajapata muda wa kuongea peke yao na dada yake mjengoni humo kwa muda mrefu sasa.
Talia alijibu kwa kusema kwamba amechoka kuishi chini ya kivuli cha dada yake na kwamba anataka kujitegemea na kuwa huru kujichanganya na washiriki wengine.
Jumapili hii rapa wa Ghana, M.anifest, atatumbuiza katika shoo ya kuwatoa washiriki.
Shoo ya Big Brother StarGame inayowaweka washiriki mjengoni kwa siku 91, imeandaliwa na kituo M-Net cha AfricaMagic, na imekuwa ikionyeshwa kwa saa 24 za siku 7 za wiki katika chaneli za 197 & 198 za Dstv.
Kwa maelezo zaidi kuhusu shoo hiyo, unaweza kuingia: www.africamagic.tv/bigbrother
No comments:
Post a Comment