SEERDOF AONDOKA AC MILAN
Clarence Seedorf |
Milan, Italia
AC Milan wamekubali kuwasajili
beki wa Chievo, Francesco Acerbi na kiungo wa Genoa, Kevin Constant lakini
kiungo wao Clarence Seedorf anaondoka katika klabu hiyo ya Serie A, Ligi Kuu ya
Italia baada ya kuitumikia kwa miaka 10, imefahamika.
Milan, waliovuliwa ubingwa wao wa
Italia na Juventus mwezi Mei, wanajenga upya kikosi chao baada ya kuondoka kwa
nyota kadhaa ‘wazee’ wakiwemo Gennaro Gattuso, Alessandro Nesta, Filippo
Inzaghi, Gianluca Zambrotta na Mark van Bommel.
Mholanzi Seedorf, aliyeng’ara
katika fainali za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2003 na 2007 wakati Milan ikitwaa
medali nne za ushindi, ameungana na kundi la wanaoondoka lakini hakusema ni
wapi anakwenda licha ya uvumi kuenea kuwa atajiunga na klabu ya Botafogo ya
Brazil.
"Kwakweli namshukuru kila
mmoja," kiungo huyo mwenye miaka 36 na ambaye hakucheza mechi nyingi msimu
uliopita, aliuambia mkutano na waandishi wa habari leo.
"Nitawaeleza hatma yangu
hivi karibuni. Naondoka. Ninatakiwa na timu nyingi sana," aliongeza
mchezaji huyo amabaye anakabidhi jezi yake namba 10 ya Milan kwa mshambuliaji
wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic.
No comments:
Post a Comment