Friday, June 29, 2012

TOM CRUISE ATALIKIANA NA MKEWE KATIE HOLMES

Katie Holmes, binti yao Suri (6) na Tom Cruise.... kimenuka!

KATIE Holmes amefungua mashitaka ya kuomba kutalikiana na mumewe nyota wa filamu Tom Cruise, ambaye "hakufahamu" kuhusu mipango hiyo ya Katie kutinga mahakamani.

Katie alifungua mashitaka hayo mjini New York jana, akiegemea kwenye "tofauti zisizosuluhishika." Ameomba pia apewe haki yote ya malezi ya binti yao mwenye umri wa miaka 6, Suri, na kubaki katika nyumba wanayoishi.

Katie pia ametaka "kiasi cha kutosha" kutoka Cruise kwa ajili ya malezi ya mtoto.

Katie pia anataka mgawanyo wa mali.

Imeelezwa kwamba Tom "hakutarajia jambo hilo litokee."  Imedaiwa kwamba huenda kuna "mchezo mchafu" katika jambo hilo ndio maana Katie amekimbilia kutaka apewe haki ya malezi ya mtoto.

Tom Cruise na Katie wakati wa raha zao

No comments:

Post a Comment