Lauryn Hill akitoka mahakamani leo |
Kwamujibu wa tovuti ya TMZ, nyota huyo wa kundi la Fugees alimweleza jaji leo kwamba kwa makusudi alikwepa kulipa kodi katika miaka ya 2005, 2006, na 2007, wakati aliingiza zaidi ya dola milioni 1.8 (sawa na Sh. Bilioni 2.8). Pamoja na kifungo cha gerezani, atapigwa faini ya dola 75,000 (sawa na Sh. milioni 116).
Wakati jaji alipomuuliza Hill kama hakulipa kodi hizo "kwa makusudi na kudhamiria", alijibu, "Ndio."
Aliachiwa kwa dhamana ya dola 150,000 (Sh. milioni 233) na atahukumiwa Novemba.
Katika barua aliyoituma katika internet, Hill alitetea matendo yake, akidai alijiondoa yeye na familia yake kwenye jamii katika kipindi hicho cha miaka mitatu ili "kuwaweka salama, wenye afya na huru mbali na hatari."
No comments:
Post a Comment