Saturday, June 30, 2012
BALOTELLI: WATU WANAONEA WIVU MWILI WANGU
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli ametetea staili yake ya kushangilia dhidi ya Ujerumani.
Balotelli alifua shati lake baada ya kufunga goli lake la pili dhidi ya Ujerumani lakini hakudokeza namna atakavyoshangilia ushindi ama goli dhidi ya Hispania katika fainali ya Euro kesho.
Balotelli alisema: "Sina cha kusema kuhusu namna nilivyoshangilia goli langu la pili.
"Mliona. Mnaweza kuhukumu. Kuna mtu alichukizwa na jinsi nilivyoshangilia goli langu la pilu?
"Kwa sababu waliona mwili wangu na wana wivu.
"Hata hivyo, sina namna maalum ya kushangilia kwenye fainali. Mimi hudumisha matumaini kwamba nitafunga. Nafikiria kufunga tu — sifikirii kuhusu kushangilia."
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment