Kocha mpya wa timu ya taifa ya vijana, Jakob Michelsen |
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtambulisha rasmi leo mbele ya
waandishi wa habari kocha mpya wa timu za Taifa za vijana, Jakob
Michelsen kutoka Denmark ambaye amechukua nafasi ya Kim Poulsen ambaye
hivi sasa anainoa Taifa Stars.
Michelsen
ambaye amepewa mkataba wa mwaka mmoja alitambulishwa na Katibu Mkuu wa
TFF, Angetile Osiah na kusema falsafa yake ni kama ile ya Poulsen ya
kumiliki mpira na kushambulia muda wote wa mchezo.
Kabla
ya kuja Tanzania, Michelsen alikuwa kocha wa timu ya daraja la kwanza
ya Hobro IK ya Denmark. Ana leseni A ya ukocha kutoka Shirikisho la
Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), leseni ya ukocha wa vijana kutoka Chama cha
Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU).
Moja
ya mafanikio yake ni kuipa ubingwa wa Denmark, timu ya Skovbakken
kwenye ligi ya timu zenye umri chini ya miaka 18. Ubingwa huo aliupata
msimu wa 2005/2006.
No comments:
Post a Comment