KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anaamini kwamba England
haitatwaa ubingwa katika michuano yoyote ya kimataifa hadi hapo itakapokubali kubadili
ratiba yake ya sasa ya ligi kuu na kuruhusu mapumziko ya majira ya baridi.
Muitalia huyo alisisitiza kwamba uchovu wa safari ndefu ya msimu
wa Ligi Kuu ya England ndio sababu kubwa ya kutolewa kwao kwa ‘matuta’ na
Italia katika robo fainali ya Euro 2012 jana.
""Fabio Capello ameifanyia makubwa England," aliiambia
Rai Radio 2.
"Na kama angekuwapo katika benchi la ufundi, bado
Italia ingelazimika kufanya kazi ya ziada."
"Nadhani wachezaji wa England wanalipa gharama
itokanayo na ukweli kwamba wamekuwa wakicheza bila kupumzika kwa miezi 10
mfululizo.
"Baadaye wanafika kwenye mashindano wakiwa taaban. Siku
zote wao hushambulia, sio kuzuia tu kama ilivyokuwa katika michuano hii ya
Ulaya."
No comments:
Post a Comment