Cristiano Ronaldo |
Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo sasa amefikia
rekodi ya muda wote ya upachikaji mabao iliyowekwa na wachezaji wa Ureno katika
fainali za Euro.
Ronaldo amekwea kileleni mwa
wafungaji wa kihistoria wa Ureno katika fainali za Euro, akiwa sambamba na Nuno
Gomes.
Hivi sasa, Ronaldo pia ni miongoni
mwa wafungaji walio kileleni katika fainali za Euro 2012 baada ya kupachika
mabao matatu na kuipeleka Ureno katika hatua ya nusu fainali, sawa na Mario
Gomez wa Ujerumani iliyofika pia nusu fainali na Alan Dzagoev na Mario Mandzukic ambao timu zao
zimeshatolewa.
No comments:
Post a Comment