LEBRON JAMES AUMIA MIAMI IKINUSA UBINGWA NBA
Ajali....! James akipiga mwereka nyuma ya mlinzi wa Oklahoma City Thunder, Derek Fisher (37) |
Yalaa...! James akisaidiwa kutoka nje ya uwanja baada ya kuumia. |
MIAMI, Marekani
LICHA ya LeBron James kushuhudia
dakika ya mwisho ya mechi akiwa benchi baada ya kuumia mguu na kutolewa nje
akiwa amebebwa, nyota huyo aliisaidia Miami Heat kushinda kwa pointi 104-98 jana
na hivyo kuongoza kwa 3-1 dhidi ya Oklahoma City katika mfululizo wa mechi zao
saba za fainali ya Ligi Kuu ya Kikapu Marekani (NBA).
Ushindi huo umeifanya Miami ikaribie
kutwaa taji la NBA kwani sasa watatakiwa kushinda mechi moja tu kati ya tatu
zilizobaki.
"Ni ushindi wa kusisimua
sana," alisema LeBron, aliyefunga pointi 26, kucheza ribaundi tisa na
kusaidia pointi 12.
LeBron alianguka na kuumia mguu wakati
zikiwa zimesalia dakika tano kabla mechi kumalizika, huku Miami ikiongoza kwa
pointi 92-90.
No comments:
Post a Comment