Wednesday, June 20, 2012

BARTHEZ, BAHANUZI, JUMA ABDUL WAANZA KUJIFUA YANGA

Ali Mustafa 'Barthez'
Barthez akiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Kaunda leo asubuhi


KIPA Ali Mustafa 'Barthez' aliyetoka klabu ya 'Wekundu wa Msimbazi', Simba ni miongoni mwa nyota watatu wapya wa Yanga walioanza kujifua na klabu hiyo ya wanajangwani kwenye uwanja wao wa Kaunda leo asubuhi na kuwa kivutio kwa mashabiki waliofika kuwashuhudia.


Wengine walioripoti leo asubuhi ni beki Juma Abdul na mshambuliaji Said Bahanuzi, ambao wote wametokea Mtibwa Sugar ambako walionyesha kiwango cha juu na kung'ara katika msimu uliomalizika wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.


Mbali na nyota hao, wengine walionogesha mazoezi ya Yanga inayojianda kutetea taji lake la michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayoanza Julai 14 ni pamoja na Nizar Khalfan aliyetua Yanga pia hivi karibuni baada ya kuachwa katika usajili wa klabu ya Philadelphia Union inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS).

No comments:

Post a Comment